ads

CHAMA cha Mapinduzi CCM wilaya ya Korogwe Mjini, kimetishia kuwatimua wanachama watakaokwenda kinyume na taratibu za chama hicho bila kujali nafasi waliyonayo, umaarufu wala uzoefu wa siku nyingi.


Akizungumza katika mkutano maalumu wa baraza la wazazi wa kujadili majina ya wagombea nafasi mbalimbali, Katibu wa CCM  Korogwe Mjini, Ally Issa  alisisitiza suala la uadilifu na kwamba hakuna mtu atakayebebwa kutokana na umaarufu wake, cheo wala uzoefu wa siku nyingi ndani ya chama ama Jumuiya zake.

Issa  alisema mchakato wa kuwapata watu wa kusimamia kura lazima ufanyike kwa umakini huku akiwataka wasimamizi hao kutenda haki.

Aidha katibu huyo alisema ndani ya chama hicho suala la rushwa halina nafasi na yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo atashughulikiwa kisheria.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: