Baraza Kuu la Waislaam Tanzania (Bakwata) limeviomba vyombo vya dola kumkamata mtu anayehubiri uislam na kudai kuwa yeye ni mtume.
Akizungumza jana Jumanne Julai 18, kwa niaba ya Mufti wa Tanzania, Msemaji wa Bakwata, Sheikh Khamis Mattaka amesema mtu huyo anayeitwa Hamza Issa anatoa mahubiri kinyume na dini ya Kiislam katika eneo la Misugusugu wilayani Kibaha.
Amesema mtu huyo anasema yeye ni Nabii Ilyasa. Amesema mtu huyo anafanya fujo kwa kutumia dini ya Kiislam na kwamba anaweza kusababisha machafuko asipochukuliwa hatua za kisheria.
"Kudai kuwa yeye ni Mtume ni upotoshaji ambao ukiachwa utasababisha vurugu,"amesema.
Post A Comment: