Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi, CUF Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kwamba hatua ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwavua Ubunge, Udiwani na kuteua wengine wapya inalenga kudhoofisha kambi ya Wabunge wa CUF na Muungano wa Ukawa.
Maalim Seif amesema, Watanzania wanapaswa wajikumbushe kwamba hata kama hicho kinachoitwa ‘kuwafukuza uanachama’ Wabunge halali wa CUF kingekuwa kiko sawa, hatua kama hiyo hufuata taratibu zote za kisheria na kikanuni za Bunge kujiridhisha kwanza.
Amesema Spika amejiridhisha vipi ikiwa hata hakuwasiliana na Katibu Mkuu wa Chama ambaye kwa mujibu wa Katiba ya CUF ndiye Mtendaji Mkuu wa shughuli za chama na pia kwa nafasi hiyo ndiye Katibu wa vikao vya Mkutano Mkuu wa Taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama
Amesema yeye kama Katibu, alimuandikia Spika Ndugai barua, Jumanne, Julai 25 akimueleza kwamba hilo lililoitwa Baraza Kuu la Uongozi la CUF halikuundwa na wajumbe halali wa Baraza Kuu.
Ameongeza kwamba, Mh Ndugai ameyapuuza yote hayo kwa sababu ni kinyume na mkakati wa Dola wa kuihujumu CUF na kuua demokrasia Tanzania.
Post A Comment: