Mbunge wa jimbo la Sengerema, William Ngeleja, amesema kutuhumiwa siyo kukutwa na hatia na maisha yanaendelea.
Ngeleja ambaye ni mmoja wa watuhumiwa waliotajwa kwenye Ripoti ya pili Rais ya kuchunguza Makinikia, ameyasema hayo leo alipokuwa akichangia Bajeti Kuu ya Serikali ya 2017/18.
Wakati akiendelea na mchango wake, aliwataka wabunge kusimama ili kuonyesha kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kupambana na wizi wa rasilimali za Watanzania ikiwamo dhahabu.
Wakati akiendelea na mchango wake huo, Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga, aliomba kutoa taarifa kwa mzungumzaji akimtaka Ngeleja kueleza uhusika wake kwenye kashfa hiyo kwa sababu kamati imemtaja.
Baada ya kauli hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, alimtaka Ngeleja kuendelea na mchango wake na kuwa alichotoa Mbunge Haonga siyo taarifa.
Hata hivyo kabla ya kuendelea na mchango wake, Ngeleja alisema ” kutuhumiwa siyo kukutwa na hatia na maisha yanaendelea”.
Post A Comment: