Wananchi wa maeneo mbalimbali nchini wamefurika kwenye televisheni kila kona kusikiliza uwasilishwaji wa ripoti ya pili ya kamati ya Rais John Magufuli kuhusu makinikia kwenye makontena 277 yaliyozuiwa bandarini.
Ripoti hiyo ambayo inawasilishwa leo Jumatatu Ikulu jijini Dar es Salaam imekuwa ikisubiriwa kwa hamu baada ya ile ya kwanza kuibua madudu yaliyosababisha Rais Magufuli kumfuta kazi aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Waandishi wetu walioko sehemu mbalimbali wameeleza kuwa wananchi maofisini na mitaani wamesimama maeneo yenye televisheni kufuatilia ripoti hiyo.
Credit - Mwananchi
Post A Comment: