ads

Klabu ya Simba SC imeanza kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa Kombe la Shirikisho la Afrika, baada ya jana kukamilisha usajili wa walinzi wawili kutoka jijini Mwanza.


Simba imevuta beki wa kushoto, Jamal Mwambeleko kutoka Mbao FC na beki wa kati Yussuf Mlipili kutoka Toto Africans ambao wote wametokea jijini Mwanza

Kwa mujibu wa Makamu wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema kwamba, Mlipili amesaini miaka mitatu na Mwambeleko amesaini miaka miwili adai mchezaji Mlipili anatua kwa mara ya kwanza kabisa Simba SC, wakati Mwambeleko yeye ni kama anarudi nyumbani sababu amewahi kuchezea timu ya vijana ya Wekundu hao wa Msimbazi.

Mbali na hilo Kaburu baada ya kukamilisha usajili huo amesema mashabiki na wapenzi wa Simba wakae mkao wa kula kwa taarifa za kuvutia zaidi kuhusu usajili wa timu yao hiyo ambao unaendelea sasa.

“Kwa ujumla nina wachezaji sita ambao wamekwishakamilisha usajili wao hapa Simba, lakini nitakuwa nachomoa mmoja mmoja namtambulisha” Alijinasibu Kaburu 

Mlipili na Mwambeleko wote waliichezea Simba SC kwa mara ya kwanza kwenye mashindano ya SportsPesa Super Cup 2017 huku Simba ikitolewa kwa penalti 5-4 na Nakuru All Stars ya Kenya.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: