ads

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amesema kama si utawala wa katiba uliopo nchini, utawala wa Rais John Magufuli ulipaswa kuendelea kuwepo miaka yote.


Mwinyi ameyasema hayo jana(Jumatatu) wakati akitoa salam za Eid El Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Amesema anayoyafanya Rais Magufuli ni mambo mazuri na kwamba kwa kiasi kikubwa amefanikiwa kulipeleka taifa mahali kuzuri.

"Amelipeleka taifa mahali kuzuri, anerudisha nidhamu, sasa hivi ukienda hospitali unapata huduma vizuri, ukienda kwenye ofisi unapata huduma nzuri," amesema. "Yako mengi mzuri, tumuunge mkono Rais wetu, kama isingekuwa katiba basi ningesema aendelee kuongoza mpaka mwisho," ameongeza.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: