ads

Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Marco (54) amepandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu ya kuishi na kufanya kazi nchini bila kuwa na  kibali.


Mwendesha Mashtaka wa Uhamiaji, Novatus Mlay alimemsomea mashtaka hayo leo Jumatano kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.

Akisoma hati ya mashtaka,  Mlay alidai kuwa  Mei 19, 2017  huko Kinondoni katika ofisi ya uhamiaji,  Marco akiwa raia wa Burundi alikutwa nchini bila kuwa na kibali cha kumuwezesha kuishi.

Marco katika shtaka la pili amedaiwa kuwa siku hiyo alikutwa akifanya kazi kama Mwanasheria Mkuu wa TBS bila ya kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya kazi hapa nchini.

Katika shtaka la tatu, Mlay alidai kuwa, Julai 6 mwaka 2011 katika ofisi ya Uhamiaji ya Dar es Salaam iliyopo Wilaya ya Ilala, mshtakiwa huyo akiwa raia wa Burundi alitoa taarifa za uongo kuhusu maelezo yake binafsi wakati akijaza fomu ya kuomba hati ya kusafiria namba CT (5)(Ai).

Wakili Mlay alisema kitendo hicho cha kutoa taarifa za uongo kilimuwezesha Marco kupata hati ya kusafiria ya Tanzania yenye namba AB 474856 huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, alikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Mshtakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh 20 milioni na alikamilisha. Kesi imeahirishwa hadi Juni 21, 2017 kwa ajili ya kutajwa.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: