ads

Baada ya kutia saini kitabu cha wageni katika ofisi yake mpya jana Alhamisi, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwhira, ameenda kuhani msiba wa aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema, mkoa huo, marehemu Philemon Ndesamburo.


Mghwira ametoa rambirambi kwa familia ya Ndesamburo, aliyewahi kuwa mbunge wa Moshi Mjini kwa awamu tatu mfululizo.

Mghwira aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli amewasili katika eneo lake jipya la kazi ikiwa ni siku mbili tu baada ya kuapishwa na Rais,  Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mghwira anaanza kazi wakati Chama cha ACT-Wazalendo kikimuondoa katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa chama hicho kutokana na matakwa ya katiba ya chama hicho.

Hata hivyo, Mgwhira ataendelea kuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: