ads

Wakati Gor Mahia ikiibuka na ushindi wa bao 3 0 dhidi ya AFC Leopard katika michuano ya SportPesa SuperCup ambapo watani hawa wa jadi kutoka Kenya walipokutana Tanzania, shabiki wa timu hiyo amemuomba Magufuli kutoa msaada kwa Raila Odinga.


Jenerali Jaro Soja ambaye ni Rais wa mashabiki wa Gor Mahia amemuomba Rais Magufuli kumsaidia mlezi wa timu yao hiyo Mhe.  Raila Odinga katika kampeni zake kama ambavyo kiongozi huyo alifanya kipindi Tanzania inafanya uchaguzi mkuu mwaka 2015 ambapo Raila Odinga alikuwa akimpa nguvu Rais John Pombe Magufuli. 

Jaro Soja anasema kuwa wao kama mashabiki wa Gor Mahia wanampenda sana Rais Magufuli kwa kuwa yeye ni rafiki mkubwa wa mlezi wao wa timu hivyo wanamkaribisha Kenya. 

Credit - EATV
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: