Katibu mkuu wa wizara ya maji, uvuvi na umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo ameibuka baada ya ripoti ya pili ya sakata la mchanga na kudai kuwa wapinzani wa Tanzania wanaugua ugonjwa wa kupinga kila kitu na kwamba wanatakiwa kumuunga mkono rais Magufuli kuokana na sakata la mchanga. Ameyatoa hayo katika moja ya akaunti zake za mitandao ya kijamii.
Aidha baada ya kutoa maoni hayo na kuwataka wapinzani kumpongeza rais Magufuli, wameibuka mashabiki wake na kumpongeza kwa kupona ugonjwa huo.
"Hongera sana ndugu Kitila, hatimaye tumegundua kuwa daktari mzuri wa kuponya ugonjwa wa kupinga kila kitu ni serikali, naona kuwa umepona kabisa baada ya kuingia kwenye matibabu ya serikali". Wameandika baadhi ya mashabiki wake wakihashiria kumpongeza.
Post A Comment: