Rais John Magufuli ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuyafuta makampuni ya simu yatakayoshindwa kujiunga na Soko la hisa la Dar es Salaam.


Rais Magufuli amesema hayo jana Juni Mosi, wakati akizindua mfumo mpya wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Pia ameziagiza taasisi za Serikali na kampuni binafsi kujiunga na mfumo wa ukusanyaji mapato ili kuiwezesha Serikali kupata kodi bila uonevu kwa upande wowote.

Rais Magufuli amesema dhamira ya Serikali ni kukusanya kodi bila kuwepo kwa malalamiko kutoka upande wowote.

Pia amepiga marufuku wizara na taasisi nyingine za Serikali kuanzisha vituo vya taarifa kwa kuwa vilivyopo ni vingi na wakati huo vinatumia gharama kubwa katika kuanzisha.

“Data Centre kama hii ni mkombozi mwingine wa kupunguza kero mbalimbali, kwa sababu ukijaza vocha yako uko Zanzibar, ukinunulia vocha yako Kigoma au Moshi, hiyo pesa inakuja TRA, hakuna mabishano” amesema


ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: