Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo aliyefariki dunia jana atazikwa Jumanne ijayo.


Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa ameliambia alisema kuwa Ndesamburo atazikwa katika makaburi ya familia nyumbani kwake eneo la Mbokomu.

Golugwa amesema Jumatatu, Juni 5 kwenye viwanja vya mashujaa mjini Moshi wananchi watapata fursa ya kuaga mwili wa Ndesamburo.

Katibu huyo amesema wakati wa kuaga mwili wake kutakuwa na salamu kutoka kwa viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, viongozi wa dini na wawakilishi wa makundi mbalimbali.

Golugwa amesema msiba wa Ndesamburo umewagusa wengi nchini kutokana na mchango wake katika kukuza misingi ya demokrasia ya vyama vingi na kuchangia ustawi wa sekta ya utalii.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: