ads

Polisi imemkamata mtuhumiwa anayedaiwa kuwajeruhi watu sita kwa kisu mjini Zanzibar Mei 29.


Mtuhumiwa huyo alikamatwa jana saa 8:30 mchana akituhumiwa kuwajeruhi watu hao katika mgahawa wa Lukmaan uliopo Mkunazini mjini Zanzibar.

Katika tukio hilo, raia wa kigeni wanne na Watanzania wawili walijeruhiwa maeneo mbalimbali ya miili yao kwa kuchomwa kwa kisu.

Mtuhumiwa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Madema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Hassan Nassir Ali amethibitisha kushikiliwa kwa mtuhumiwa huyo.

Amesema wanaendelea kumhoji ikiwa ni hatua za awali za upelelezi.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: