Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Mei wa ligi ya Hispania (La Liga) huku Zinedine Zidane akishinda tuzo ya meneja bora.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 ameshinda tuzo hiyo, baada ya kufunga mabao matano katika michezo minne ya mwisho na kuisaidia Real Madrid kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa La Liga baada ya miaka mitano.
Zidane ametangazwa kuwa meneja bora wa mwezi Mei, baada ya kuiongoza Real Madrid kushinda michezo ya mwezi huo na kuwapiku wapinzani wake Barcelona kwenye mbio za ubingwa wa La Liga.
Wawili hao wanaendelea kuchagiza furaha ya mashabiki wa klabu ya Real Madrid, ambayo iliendelezwa mwishoni mwa juma lililopita, kwa kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, kwa kuifunga Juventus mabao manne kwa moja.
Post A Comment: