ads

Baada ya wiki iliyopita kusambaa picha mitandaoni za muimbaji Christian Bella zikimuonyesha akiwa amelazwa hospitali nchini Congo na kuzua hofu kwa mashabiki wa muziki wake, muimbaji huyo amefunguka kuzungumzia kitu ambacho kilimsibu.


Akiongea Ijumaa hii, Bella amesema alikimbizwa hospitali baada ya kuishiwa nguvu ghafla.

“Namshukuru Mungu anaendelea vizuri, nililazwa kwa muda mfupi kutokana na uchovu lakini baada ya kufanyiwa vipimo nilikutwa nimechoka tu. Kwahiyo baada ya kupumzika niliruhusiwa lakini niliambiwa natakiwa nitenge muda wa kumpumzika kwa sababu nilikuwa na tour ya muda mrefu kwa hiyo mwili ulikuwa umechoka sana,” alisema Bella.

Muimbaji huyo ambaye ni raia wa Congo, kwa sasa amerejea nchini Tanzania kwaajili ya kuendelea na shughuli zake za muziki baada ya kuwa na tour kubwa ya nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Kati.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: