Balozi wa China nchini, Lu Youging amempongeza Rais John Magufuli na Serikali kwa bajeti nzuri iliyowasilishwa jana, Juni 8 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango.
Balozi Youging ametoa pongezi hizo jana (Ijumaa) Ikulu jijini hapa alikokwenda kufanya mazungumzo na Rais.
Amesema bajeti hiyo imeakisi dhamira za kuongeza kasi ya maendeleo katika sekta mbalimbali za ikiwamo ya ujenzi na miundombinu.
“Lakini pamoja na bajeti nzuri kuwasilishwa uchumi wa Tanzania umeendelea kuimarika na kuwavutia wadau wengi wa maendeleo kuwekeza nchini,” amesema.
Ameongeza kuwa Tanzania inapewa kipaumbele na nchi ya China na kwamba Serikali ya nchi hiyo itaendelea kuwashawishi wawekezaji wengi zaidi kuwekeza hapa nchini.
Post A Comment: