BAADA ya kundi la Yamoto Band kusambaratika na wasanii wake, Enock Bella, Aslay, Beka na Maromboso kila mmoja kupata menejimenti yake mpya na kuanza kufanya kazi kama ‘solo artists’, hatimaye Beka 1 Flavour anayetamba na ngoma yake ya Libebe ameibuka na kujibu tuhuma zinazowakabili kuwa licha ya kupewa nyumba na meneja wao wa Yamoto Band, Mkubwa Fella, bado wamemkimbia.
“Yamoto Band bado ipo isipokuwa Mkubwa mwenyewe ametupa ‘go ahead’ ya kufanya kazi kama ‘solo artists’ na kuhusu kupewa nyumba Mkubwa hajatugawia nyumba isipokuwa yale ni mavuno ya tulichokipanda baada ya kufanya shoo nyingi ndani na nje ya nchi na kuingiza mtonyo wa kutosha ndipo tukakaa na kujadili kwamba badala ya kutugawia malipo yetu, kila mmoja tukaona ni bora atusimamie tuweze kusimamisha vibanda vyetu,” amesema Beka1 Flavour.
Post A Comment: