Serikali imesema bajeti ya mwaka huu inajibu hoja zilizojadiliwa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inayosisitiza kuhusu uchumi wa viwanda.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema uchumi unaolengwa na nchi wanachama wa EAC ni ule unaotaka kukuza viwanda na hivyo tayari Tanzania imeweka mikakati ya kufikia malengo hayo.
Miongoni mwa mambo ambayo Tanzania imekusudia kuyatilia mkazo kwenye bajeti yake ni kuongeza makusanyo ya ndani, kupunguza mfumuko wa bei, kufuta misamaha ya kodi inayotolewa kiholela na kuweka sera nzuri ya kodi.
Maeneo mengine ambayo yameainishwa na Dk Mpango ni kuongeza mapato yasiyokuwa ya kodi, kuweka tathmini na kuhusu kodi ya majengo na kuimarisha soko la ndani.
“Sera hii ikiwamo kuanzisha mfumo rasmi wa ukusanyaji kodi kwa njia ya kielektroniki itasaidia kwa sehemu kubwa kuongeza mapato ya ndani,” amesema.
Post A Comment: