ads

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango amesema serikali itaendelea kuliboresha shirika lake la ndege nchini ATCL ikiwa ni pamoja na kuchukua madeni yake mbalimbali ili kuhakikisha shirika hilo linafanya kazi kama ilivyokusudiwa .


Dkt Mpango ametoa kauli hiyo wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia bajeti ya Wizara hiyo ya fedha kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.

“Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali amekamilisha ukaguzi wa shirika letu la ndege, ilikukamilimisha mizania ya kampuni, lakini tumeamua kuyachukua madeni yote ya ATCL ili kuweza kusafisha hiyo mizania,” alisema Dkt Mpango.

“Muheshimiwa Rais ameteua bodi mpya ya wakurugenzi ambayo inaweledi katika mambo ya usafirishaji wa anga, menejimenti mpya lakini kuhakikisha shirika linakuwa na mpango wa biashara wa muda wa kipindi cha kuanzia mwezi Julai mpaka mwezi Juni mwaka huu.”
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: