ads

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa amewatakia mfungo mwema wa Ramadhani Waislamu wote akiwaomba kutumia ibada zao kuwaombea viongozi wa nchi hekima na busara na kuombea nchi amani na utulivu.


Waumini hao wanatarajiwa kuanza mfungo mtukufu wa Ramadhani Jumamosi baada ya mwezi kuandama.

Lowassa amesema kuanza kwa mfungo huo ni kutekeleza moja ya ibada zao muhimu kwa waumini hao.

“Ni kipindi ambacho Waislamu wanatakiwa kutenda mema zaidi na kuwa karibu zaidi na mwenyezi Mungu kwani malipo katika mwezi huu ni mara dufu zaidi ya miezi mingine.”

“Nachukua nafasi hii kuwatakia ndugu zangu Waislamu mfungo mwema katika mwezi huo mtukufu wa Ramadhani, na kuwaomba wafanyabiashara kutopandisha bei za vyakula katika mwezi. Pia nawaomba  ndugu zetu akristo na wa dini nyingine kuwa na ushirikiano na wenzao kama ilivyo desturi yetu, ili watimize ibada hii muhimu kwao.”

“Kwa wale wenye uwezo tuwasaidie wenzetu wasiyokuwa nao na pia katika ibada zetu tuiombee nchi yetu amani na utulivu  na pia kuomba hekima na busara zitawale ndani ya vichwa vya viongozi wetu,”amesema Lowassa.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: