ads

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amekemea vikali mauaji yanayotokea mkoani Pwani.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo, Alhamisi   Polepole amesema kuwa kama CCM wanataka kuona mauaji hayo yanaendelea kukemewa zaidi.

Polepole ameonyesha  masikitiko yake kwa vyama vya upinzani kukaa kimya badala ya kuungana kama Taifa kukemea mauaji ya watendaji wa CCM yanayoendelea mkoani Pwani.

"Kuungana kwenye ruzuku, hapana vyama vinapaswa kuwa na umoja katika masuala mbalimbali ikiwamo mauaji hayo," amesema Polepole.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: