Habari za leo wapendwa
Cancer ya utumbo mkubwa (Colon Cancer) ni ya tatu duniani kwa kusababisha vifo ukitoa breast na lung cancer. Dalili za cancer hii ni pamoja na kupungua damu, kutoa damu katika njia ya haja kubwa, maumivu yanayodumu kwa sekunde mbili na kuondoka, kubadilika kwa ratiba yakupata haja kubwa, kupungua kwa uzito wa mwili.
Vitu vinavyosababisha cancer hii kwa wengine na kurithi kutoka kwenye genes, lakini kwa wengine wengi ni ugonjwa wa diabetes type 2 usiodhibitiwa, ulaji wa vyakula vya wanga na mafuta, kuto kufanya mazoezi, kutokula vyakula vya fiber kama (ugali wa dona, maharage, makande nk), unywaji wa pombe uliopitiliza, nk.
Ugonjwa huu hasa hutokea kwa watu wa miaka 60 na kuendelea lakini kwa siku za karibuni umri wa wagonjwa unazidi kushuka, inawezekana (life style) kuwa sababu kubwa. Mara nyingi mgonjwa wa colon cancer anapogundulika 25% inakuwa imeshafikia kwenye secondary stage.
jinsi ugonjwa wa kansa ya tumbo unavyopimwa |
Post A Comment: