Klabu ya Simba imepewa rasmi pointi 3 na mabao matatu baada ya kushinda rufaa yake dhidi ya Kagera Sugar wanaodaiwa kumtumia mchezaji aliyekuwa na kadi tatu za njano kinyume cha kanuni.
Maamuzi hayo yamefanywa na Kamati ya Saa 72 ya TFF, baada ya kupitia rufaa ya Simba na kujiridhisha kuwa ni kweli mchezaji anayelalamikiwa alikuwa na kadi tatu za njano lakini bado alipangwa kucheza katika mchezo uliowakutanisha Simba na Kagera Sugar Mjini Bukoba.
Taarifa iliyotolewa na TFF kuhusu maamuzi hayo usiku huu imesema "Kikao cha Kamati ya Saa 72, kimethibitisha kuwa mchezaji Fakhi Mohammed alikuwa na kadi tatu hivyo Kagera Sugar inaporwa pointi tatu na magoli matatu kwa mujibu wa kanuni ya 37 (37) kwa kosa la kanuni ya 37 (4)"
Taarifa hiyo imesema kuwa Fakhi alipata kadi za njano katika mechi kati ya Kagera na Mbeya City, Kagera Sugar na Majimaji na Kagera Sugar na Africa Lyon
Kamati hiyo pia imesema imechukua muda mrefu kufanya maamuzi kwa ajili ya kukusanya ushahidi ili kujiridhisha baada ya Kagera Sugar kupinga malalamiko ya Simba.
Katika mchezo ule Simba ilifungwa mabao 2-1.
Maamuzi hayo yataifanya Simba iweze kufikisha point 61 na kujikita zaidi kileleni ikifuatiwa na Yanga ambayo ina mchezo mmoja mkoni, ikiwa na pointi 56.
Post A Comment: