ads

Sakata la pointi tatu ambazo Simba SC ilipewa na Kamati ya Saa 72 kutokana na kile kinachodaiwa Kagera Sugar ilichezesha mchezaji Mohamed Fakhi akiwa na kadi za njano tatu kinyume na sheria za ligi kuu msimu 2016/17 limechukua sura nyingine baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania kusema bado ushahidi haujakamilika ipasavyo hivyo.


Akitangaza mbele ya waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa amesema kikao cha jana kilikuwa maalumu kwa ajili ya kumaliza kazi ilianzwa na Kamati ya Saa 72 na sio kuiharibu maamuzi yake ambayo ilitoa.

“Mashahidi wengi hawajaweza kufika hivyo lazima usubiri mpaka waletwe ili kukamilisha kazi. Pia nyaraka muhimu haziletwa. Kamati ya Saa 72 haina nguvu ya kustafiri sheria hivyo kinachofanyika sisi (Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji) tunamalizia ilipoishia,” alisema Mwesigwa.

Mwesigwa ameongeza kuwa ni lazima kuliweka suala hili vizuri kwa maslahi ya siku za usoni hivyo wakienda nalo kwa pupa litakuwa na athari katika siku zijazo katika soka la Tanzania.

Kikao hicho kimeahirishwa hadi leo Aprili 19 mwaka huu.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: