Msanii wa filamu nchini Jacob Stephen maarufu kama JB amefunguka na kusema kuwa kikosi cha Simba cha hivi sasa si kibaya sana ukilinganisha na vikosi kadhaa vya Simba ambavyo yeye anavikubali zaidi.
JB anadai kuwa katika moja ya vikosi vya Simba ambavyo vimewahi kumkosha sana ni pamoja na kile kikosi kilichoipiga Yanga bao 4
"Simba ambayo ilinifurahisha naikumbuka ni ile Simba ya CAF, iliyofika fainali ya CAF Simba ile niliipenda sana ile ilikuwa ni Simba bora kwangu mimi, harafu nyuma yake baada ya ile Simba nyingine iliyokuwa nzuri ni ile ya Captain aliyemaliza muda wake Seleman Matola nayo ilikuwa Simba nzuri sana ambayo kwa mara ya kwanza iliweza kuwatoa waarabu kama unakumbuka ni Simba ambayo ilinifurahisha mno" alisema JB
JB alizidi kufafanua vikosi vya Simba ambavyo kwake vilimkosha kuwa ni pamoja na Simba ile ambayo Okwi aliingia kwa mara ya kwanza.
"Simba ya Okwi wakati anaingia kwa mara ya kwanza ilikuwa nzuri sana, Simba ile iliyopiga Yanga goli 4 ilikuwa Simba nzuri, na hata hii Simba tuliyonayo saizi si Simba mbaya sana lakini zile za nyuma nadhani zilikuwa katika ubora wake zaidi" JB
Post A Comment: