Serikali imekiri kuwepo kwa ongezeko la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani hasa katika miji mikubwa nchini ambapo takwimu zinaonesha kuwa Jiji la Dar es salaam linaongoza kwa asilimia 28 ya watoto hao nchini
Hayo yamebainishwa leo Bungeni na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akijibu swali la Mhe Khatib Said Haji Mbunge wa jimbo la Konde aliyetaka kujua serikali inachukua hatua gani kukabiliana na ongezeko la watoto wa mtaani.
"Ni kweli kumekuwa na ongezeko la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani hasa katika miji mikubwa. Kwa mujibu wa takwimu zilizofanyika katika miji ya Dar es Salaam na Mwanza mwaka 2012 zilionesha kuwa Jiji la Dar es Salaam lilikuwa na watoto 5,600 kutoka mikoa 10 ambayo ni Dar es Salaam 28%, Dodoma 8%, Mwanza 7%, Morogoro 7%, Tanga 6%, Iringa 5% Pwani 5%, Kilimanjaro 5% , Arusha 4%". Alisema Waziri Ummy
Aidha Waziri huyo amesema serikali ina jukumu la msingi la kuhakisha ulinzi na usalama kwa watoto hao unapatikana pamoja na kushirikisha jamii iweze kuwasaidia kuwaokoa vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi wakiwemo watoto wa mtaani.
Post A Comment: