ads

. Ayoub Mwaikambo, askari aliyeuawa katika shambulio dhidi ya gari la Jeshi la Polisi wilayani Kibiti, ameacha mke ambaye anatarajiwa kujifungua mwezi mmoja ujao.

Hayo yamebainika katika hafla ya kuaga miili ya askari nane waliouawa katika shambulio lililotokea Alhamisi jioni, huku kukiwa na taarifa nyingine ya kushambuliwa kwa mapanga kwa mtoto wa mwenyekiti wa Kijiji cha Kitembo wilayani Kibiti ambako mauaji dhidi ya viongozi na askari yanazidi kuongezeka.

Mtoto huyo, Saidi Abdallah alijeruhiwa kwa mapanga baada ya kukataa kuwatajia watu waliovamia nyumba yao usiku wa kuamkia jana, sehemu aliyojificha baba yake ambaye ni mwenyekiti wa kijiji hicho.

Jana, wakati wa hafla ya kuaga miili ya askari hao iliyofanyika Kurasini Barracks, Francisco Mwaikambo, ambaye ni kaka wa askari huyo, alisema amempoteza mtu ambaye alikuwa akijadiliana naye mambo ya familia.

“Ah! Ayoub amekufa wakati nilikuwa nimepata mtu mwingine wa kujadiliana naye mambo ya familia baada ya kukua na kufahamu umuhimu wa familia,” alisema Francisco huku midomo ikimcheza mithili ya mtu anayejizuia kulia. “Amemuacha mtoto wake tumboni.”
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: