WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
amesema kwamba kuanzia wiki ijayo wizara yake itawatangaza hadharani
watu wote ambao wamekwepa kulipa kodi ya ardhi na majengo, wakiwemo
vigogo walioko serikalini.
Akifungua semina juu ya jukumu la vyombo vya habari katika kutoa
elimu ya sheria, kanuni na taratibu katika utawala wa ardhi ili kusaidia
kutatua migogoro, iliyofanyika mjini hapa, Lukuvi alisema kwamba
watayatangaza majina hayo ili watu wawajue watu wanaojenga majumba ya
kifahari lakini hataki kulipa kodi ya serikali.
“Tutatangaza majina yao halisi sio yale ya bandia, ili watu wawajue
kuwa kuna watu wamejenga majumba ya fahari, lakini hawalipi kodi ya
serikali, baada ya kutangaza tutawapiga faini. Na mwakani tutaweka kodi
kubwa zaidi kwa mashamba na viwanja visivyoendelezwa,” alisema Lukuvi.
Alisema gharama ya kodi, pia imepunguzwa kutoka Sh 1,000 na sasa mtu
atalipia ekari moja kwa Sh 400.
“Nani huyo asiyeweza kulipia kiasi hicho
cha fedha,” alihoji.
Alisema wizara yake inaangalia hata wale ambao wanamiliki kimila, nao
wachangie kidogo, kwa sasa hawalipii hata kidogo Kuhusu hoja ya
kuwanyang’anya watu mashamba ambayo hayajaendelezwa, alisema serikali
haitaangalia cheo, jina wala wadhifa wa mtu, badala yake wale wote wenye
mashamba ambayo hajaendelezwa watanyang’anywa.
Alisema kama kuna kiongozi yeyote serikali au kigogo mstaafu, ambaye
amehodhi ardhi katika mkoa wowote na hajaiendeleza, huyo atahesabiwa
amekiuka masharti ya kumilikishwa ardhi na hivyo lazima achang’anywe.
Alisema kabla ya kufuta hati ya umiliki, Serikali inatoa notisi ya
kufuta kabla ya kufanya hivyo kwa viwanja na mashamba, sasa mchakato
ukiiva baada ya siku 90 kama utetezi wake hauridhishi, anampelekea rais
anafuta hati hizo za umiliki.“Hakuna atakayepona katika mpango huu,”
alisema Lukuvi.
Alishauri taasisi za serikali kutumia wapima ardhi binafsi kwani ni
waadilifu kuliko wale wa serikali, “Wapima binafsi ni waadilifu, mkiwapa
kazi maeneo yetu yatapona, mkiwapa viwanja 1,000 watakurudishia viwanja
vyote, ila aliyeajiriwa na halmashauri atakurudishia viwanja 500,
viwanja 500 ‘atavipiga’. Na ‘upigaji’ wao ni ufundi haswa.”
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: