Watoto
61 wamezaliwa katika hospitali nne jijini hapa wakati wa mkesha wa
Sikukuu ya Krismasi, kati yao wa kiume wakiwa 36 na wa kike 25.
Takwimu
kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) zimeeleza watoto tisa
walizaliwa hospitalini hapo, kati yao wa kiume ni watano na wa kike
wanne. Katika Hospitali ya Amana, walizaliwa watoto 28, wa kiume wakiwa
16 na wa kike 12, huku watano wakizaliwa kwa njia ya upasuaji.
Hospitali
ya Mwananyamala walizaliwa watoto 16 kati yao wa kiume wakiwa wanane na
wa kike wanane, mtoto mmoja akizaliwa kwa njia ya upasuaji; huku watoto
wanane, wa kike saba na wa kiume mmoja walizaliwa kwenye Hospitali ya
Temeke.
Ofisa
muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Amana, Theresia Akida alisema
watoto waliozaliwa hospitalini hapo wana afya njema na wanaendelea
vizuri.
Katika
Hospitali ya Temeke, Ofisa Muuguzi Hamisa Shaabani, alisema kati ya
watoto wanane waliozaliwa, kuna pacha. Alisema hali za watoto na wazazi
zilikuwa njema na waliruhusiwa kutoka hospitalini.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: