MMCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo jijini Dar es
Salaam, Anthony Lusekelo maarufu 'Mzee wa Upako, aliwagomea waandishi wa
habari kusikiliza hotuba yake ya ibada na kutuma wasaidizi wake
wawaondoe waandishi hao.
“Samahani tunaomba muondoke kwani Mchungaji amesema hataki kumuona
mwandishi hivyo tunaomba muende kwenye makanisa mengine,” alisema
msaidizi huyo na kuhakikisha waandishi wote wanaondoka eneo hilo majira
ya saa sita kasoro mchana.
Lusekelo maarufu Mzee wa Upako hivi karibuni amekuwa akirushiana
maneno na baadhi ya waandishi wa habari baada ya kuandikwa akituhumiwa
kuwa mlevi na kutukana hadharani.
Desemba 25 ya kila mwaka, waumini wa dini ya Kikristo nchini huungana
na wenzao duniani kuadhimisha sherehe za kuzaliwa kwa Bwana wao Yesu
Kristo yapata miaka 2000 iliyopita.
Wakati huohuo waumini wa dini ya Kikristo nchini wametakiwa kudumisha
upendo, utii na unyenyekevu ili kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa
Bwana na Mwokozi wao Yesu Kristo ikiwa ni pamoja na kuliombea amani
taifa lao la Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ibada ya mkesha
wa sikukuu hiyo, Dk Alex Malasusa, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, aliwataka
waumini wa kanisa hilo, kuhakikisha wanakuwa mabalozi wa amani na upendo
kwa wenzao.
Alisema siku ya Krismasi ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwana wa Mungu
Yesu Kristo ambaye kutokana na upendo wake, aliwaunganisha watu na
Mwenyezi Mungu.
“Tuuenzi upendo wake, lakini kubwa zaidi tukumbuke kuwa amani ndio
msingi wa sikukuu hii. Hata alipokuja Yesu maneno yake ya kwanza
yalikuwa ni amani,” alisisitiza. Askofu Malasusa, aliwataka wananchi
katika kudumisha upendo huo, waliombee taifa pamoja na viongozi wake ili
amani iliyopo iendelee kudumu.
“Ndio maana leo katika ibada yetu ya mkesha wa Krismasi tumeamua
kupeana zawadi ikiwa ni ishara ya kuoneshana upendo na kudumisha amani
miongoni mwetu,” alisema.
Mara baada ya ibada hiyo, waumini wa kanisa hilo, walibadilishana
zawadi ambayo kila mtu alikuja nayo na kumpatia mwenzake huku Askofu
Malasusa na viongozi wengine wa Kanisa hilo nao wakigawa zawadi zao kwa
waumini hao.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: