SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema
haina mpango wa kuwazuia viongozi wastaafu kugombea urais wa visiwa
hivyo pamoja na kwamba wananufaika na mafao ya nyadhifa zao walizokuwa
wakizitumikia akiwamo aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif
Sharif Hamad.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi (BLM), Issa Haji Gavu, alipokua akijibu swali la
Mwakilishi wa Mfenesini, Machano Othman Said, katika kikao cha Baraza la
Wawakilishi jana.
Alisema sheria namba 2 ya 2012 imeanzishwa kwa madhumuni ya kuwaenzi
na kuwatunza viongozi wastaafu Zanzibar kwa kutambua mchango wao katika
kulitumikia taifa na wananchi wake.
“Sheria hii haikuzungumzia suala la kuwakataza viongozi hao
kutogombea nafasi nyengine za uongozi katika serikali kupitia vyama vyao
baada ya kustaafu.”
"Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi lazima mfahamu suala la kuchagua
na kuchaguliwa ni haki ya kikatiba kwa kila mwananchi aliyefikia vigezo
vilivyowekwa kwa mujibu wa kifungu cha 26 (a) (d) cha Katiba ya Zanzibar
ya 1984.
Wakati huu serikali haioni busara ya kuwabana kisheria viongozi wa
kisiasa wastaafu wasitumie fursa yao ya kikatiba kugombea uongozi pale
wanapoona inafaa,” alisema Gavu.
Aidha, w
aziri huyo alisema haki ya kuwalipa viongozi wa kisiasa
wastaafu ni jambo la kisheria na halitokani na utashi, hivyo serikali
itaendelea kuwalipa na kuwapa haki zao nyengine viongozi hao kama sheria
ilivyosema.
Pia alisema serikali haina wazo la kuwa na baraza la ushauri la
viongozi wastaafu kwani Rais hakwaziki kutaka ushauri kwa mtu yoyote na
wala halazimiki kufuata ushauri wa mtu yoyote katika utekelezaji wa
majukumu yake.
Viongozi ambao wamestaafu nyadhifa za juu serikalini visiwani hapa na
wamekua wakiwania nafasi ya urais wa ni Maalim Seif (CUF) na aliyekuwa
Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha (CCM).
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: