Klabu ya Simba imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kocha wa makipa Iddi Salim Raia wa Kenya ikiwa ni mara yake ya pili kuinoa Simba.
Kocha huyu mwenye uzoefu katika kazi yake alitumbuliwa na Simba akiwa pamoja na kocha wa kipindi kile Mwingereza Dylan Kerr baada ya kufanya vibaya hivyo wote walitupiwa virago.
Safari hii amerejea
Simba akiwa amejifua zaidi na kupata leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya
(Uefa), maana yake anaweza kufanya kazi Barani Ulaya.
Kocha huyu pia
alishawahi kufanya kazi na Mabingwa wa Zamani wa Kenya timu ya Gor
Mahia, AFC Leopards za Kenya pamoja na timu ya taifa ya nchini hiyo,
Harambee Stars.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI


Post A Comment: