
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Balozi Augustine Mahiga (kushoto) kwa pamoja na Mhe.
Reem Ebrahim Al Hashimy, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Ushirikiano wa
Kimataifa wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wakisaini Mkataba wa Ushirikiano katika Sekta ya Anga. Mkataba huo ulisainiwa wakati wa kikao
cha kwanza cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kilichofanyika
Abu Dhabi, Falme za Kiarabu tarehe 19 na 20, Desemba, 2016.
………………………………………………………………….
Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) zimefanya
kikao cha kwanza cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano huko Abu
Dhabi makao makuu ya Umoja wa Falme za Kiarabu. Kikao hicho kilifanyika
tarehe 19 na 20, Desemba, 2016
Mkutano huo ulioshirikisha sekta
mbalimbali za Serikali zote mbili uliongozwa na Mhe. Dkt. Augustine
Mahiga (MP), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
wa Tanzania na Mhe. Reem Ebrahim Al Hashimy, Waziri wa Nchi
anayeshughulikia Ushirikiano wa Kimataifa wa Umoja wa Falme za Kiarabu
(UAE).
Pamoja na mambo mengine, katika
mkutano huo Tanzania na UAE zimekubaliana kushirikiana kwenye masuala ya
Kidiplomasia; Uchumi; Utalii; Nishati; Kilimo; Sayansi na Teknolojia;
Usafirishaji; Miundombinu; Ulinzi na Usalama; Elimu pamoja na Kazi na
Ajira.
Sambamba na mkutano huo, Tanzania
na UAE zimesaini Mkataba wa Ushirikiano katika Sekta ya Anga (Bilateral
Air Service Agreement-BASA) na Mkataba wa Ushirikiano katika Sekta ya
Utalii. Vilevile Serikali zote mbili zimekubaliana kukamilisha na
kusaini Mkataba wa Kutotoza Kodi Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji wa Kodi
za Mapato; Mkataba wa Kuhamasisha na Kulinda Uwekezaji; pamoja na
ushirikiano katika sekta ya Elimu, Afya, Ulinzi na Usalama, Ushirikiano
katika Usafiri wa Majini, Kazi na Ajira pamoja ushirikiano katika
masuala ya Zimamoto na Uokoaji.
Mkutano huo umekuwa ni chachu
katika mahusiano ya kihistoria ya nchi hizi mbili ambapo umeweka
mazingira rasmi ya ushirikiano sio tu kwa Serikali bali pia kwa sekta
binafsi.
Mheshimiwa Waziri Mahiga katika
hotuba yake ya ufungaji alitoa wito kwa Jumuiya za Wafanyabiashara na
sekta binafsi kwa ujumla za Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu
kuchangamkia fursa zinazopatikana katika nchi hizi mbili kuafuatia
mkutano huo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 21 Desemba, 2016.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: