Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa ufafanuzi kuhusu miili 7 ya watu
iliyokutwa ikielea katika mto Ruvu na kusema kuwa linaendelea na
upelelezi kwa lengo la kuwatambua marehemu hao.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi
wa Upelelezi wa makosa ya JInai Kamishna wa Polisi Robert Boaz, amesema
jeshi hilo bado halijawatambua marehemu hao, huku akitetea uamuzi wa
jeshi hilo kuzika haraka miili ya marehemu 6 kati ya 7.
"Hatua zote za kitaalam zilifuatwa na tunaendelea kufanya upelelezi
unaolenga kuwatambua marehemu hao na kujua ni jambo gani liliwasibu,
tunawasihi wananchi kuendelea kutupa taarifa zitakazosaidia kutambulika
kwa marehemu hao" Amesema Boaz
Akielezea jinsi jeshi hilo lilivyopata taarifa, amesema jeshi hilo
lilipata taarifa za kuelea kwa maiti 7 katika mto Ruvu eneo la Mkuruge
wilayani Bagamoyo kati ya tarehe 6/12/2016 hadi 9/12/2016 ambapo askari
na daktari walifika katika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa
kitaalam.
Amesema miili 6 kati ya 7 ilikuwa imeharibika sana na ndiyo maana
iliamuliwa zizikwe katika eneo la tukio wakati moja yenye unafuu
ikipelekwa hospitali ya wilaya ya Bagamoyo hadi tarehe 16/12/2016
ilipozikwa na halmashauri baada ya kutotambuliwa na tu yoyote.
Kuhusu kutoweka kwa msaidizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Ben
Sanane, Kamishna Boaz amesema jeshi hilo linaendelea na upelelezi ili
kubaini mahali alipo na kilichomsibu.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI


Post A Comment: