ads

KIUNGO wa Yanga, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, amesema mbinu za kocha wao George Lwandamina zitawafanya wasishikike baada ya siku chache kuanzia sasa.


Niyonzima ametoa kauli hiyo siku chache baada ya mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu dhidi ya JKT Ruvu ambayo walishinda kwa mabao 3-0.

"Mimi naiona Yanga nyingine, kocha ameongeza mbinu na kutupa makali na hili litaonekana kwenye mzunguko wa pili unaoendelea," alisema Niyonzima.

Alisema kikosi chao kinauwezo wa kufanya vizuri zaidi ya yale waliyoyaonyesha kwenye mchezo uliopita ambao ulichezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 

Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Rwanda, alisema kama kila mchezaji atafuata wanachofundishwa kwenye mazoezi wananafasi kubwa ya kutetea ubingwa wao.

Niyonzima amerejea kwenye kiwango chake cha juu cha uchezaji ambapo katika mchezo wa juzi alionyesha uwezo mkubwa na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi huo uliowafanya waendelee kuifukuza kwa karibu Simba inayoongoza ligi.

Timu hizo zimepishana kwa pointi mbili huku Simba ikiongoza kwa pointi 38 baada ya timu zote kucheza michezo 16.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: