UONGOZI wa Simba umesema wachezaji wake Waghana kipa Daniel Agyei na
kiungo James Kotei wana vibali vya kufanya kazi ndio maana waliwacheza
mchezo dhidi ya Ndanda FC mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akizungumza jana, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara
amewataka mashabiki na wapenzi wa Simba kupuuza habari zinazodai kwamba
watapokwa pointi kwa kuwatumia wachezaji hao wakiwa hawana vibali vya
kufanya kazi.
“Ndanda wasifikiri Simba inaongozwa na watu wasiojua taratibu hadi
tuwachezeshe wachezaji bila vibali, acha wapeleke rufaa yao Bodi ya
Ligi, watapewa majibu huko,” alisema Manara.
Ndanda FC imekata rufaa Bodi ya Ligi ikipinga Simba kuwachezesha
wachezaji hao katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Nangwanda
Sijaona Mtwara ambapo Simba ilishinda mabao 2-0.
Akizungumzia sakata hilo jana, Katibu wa Ndanda, Suleiman Kachele
alisema wana uhakika kwamba wachezaji hao walichezeshwa pasi na vibali
vya kufanya kazi.
“Sisi tumekata rufaa kwa kuwa Simba iliwachezesha wachezaji ambao
hawakuwa na vibali na sasa tunasubiri matokeo na matarajio yetu haki
itatendeka tutapewa pointi tatu,” alisema Kachele.
Akifafanua suala la kikanuni kwa mchezaji aliyecheza mechi bila
kibali cha kufanya kazi, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Hamad Yahaya
alisema:
“Kanuni zinasema kama mchezaji wa kigeni atacheza bila kibali cha
kufanya kazi ataadhibiwa kwa kufungiwa, lakini sio timu kupokwa pointi”.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: