ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp
Kardinali Pengo amewashangaa watu wanaolalamika maisha ni magumu wakati
serikali ya awamu ya tano imejitahidi kuboresha miundombinu yenye
kuleta unafuu wa maisha.
Katika salamu zake za Krismasi kwa Watanzania, Askofu Pengo alisema
hali ya maisha kwa sasa imeboreka zaidi kwani barabara nyingi
zimetengenezwa kurahisishia usafirishaji wa biashara kati ya nchi na
nchi jirani na kati ya mkoa na mkoa.
Pia alisema kitendo cha Serikali kununua ndege kadhaa kwa ajili ya
Kampuni ya Ndege (ATCL) kumerahisisha maisha ya Mtanzania kwani
kunawezesha watu kusafiri kwa haraka kwa gharama ndogo.
"Kwa mfano Arusha kwa ndege tulikuwa tunaenda kwa Sh 800,000, lakini
sasa hivi unaweza kwenda kwa gharama kati ya Sh 360,000 na Sh 400,000
kwa kutumia ndege za Serikali, napata shida kusema hali ya maisha ni
ngumu," alisema Askofu Pengo.
Kuhusu amani Pengo alisema katika awamu hii ya tano, kuna amani kubwa
na akatoa mfano wa kisiwani Zanzibar kuwa siku za nyuma watu waliishi
kwa wasiwasi mkubwa kutokana na watu kumwagiwa tindikali na viongozi wa
dini ya Kikristo kupigwa risasi, lakini sasa hivi kuna amani kuliko
wakati uliopita.
"Kule Zanzibar, hali ilikuwa ya kutia mashaka, sisi hatukujua
tukimbilie wapi kutokana na mashambulizi yale yaliyolenga watu wa dini
moja, lakini kwa sasa amani ni kubwa zaidi kuliko awamu iliyopita,"
alisema Askofu Mkuu Pengo.
Aliwakumbusha Watanzania kwamba kila mtu akisimama na kutambua wajibu
wake wa kudai amani, hali itakuwa nzuri zaidi. Pia alitoa mwito
Watanzania wasifarakane kwa sababu ya dini na akawataka waamini wa
Kikatoliki wawe wa kwanza kutetea amani na mapatano dhidi ya watu wa
dini nyingine.
Pia alisema pamoja na tofauti za dini na itikadi za kisiasa, Wakatoliki wanatakiwa kuwa na msimamo wa kutetea umoja na amani.
Asema amani italetwa na masikini, si matajiri
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: