MLINZI wa shamba moja la minazi katika Kata
ya Nyengedi, mkoani Lindi, Athanas Fulko (38), ameuawa kikatili kwa
kuchinjwa mithiri ya mnyama na watu wasiofahamika kisha mwili wake
kuutelekeza kando ya barabara kuu ya Masasi- Lindi.
Fulko,
mwenyekiji wa Kijiji cha Rondo Mitanga, alikuwa anafanya kazi ya ulinzi
kwenye shamba hilo linalodaiwa kumilikiwa na familia ya Lisuma,
inayoishi Kata ya Mtama mkoani Lindi.
Habari zilizothbitishwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ngazi ya kata na mkoa juzi zilisema mlinzi huyo alikutwa na umauti usiku wa Desemba 25, mwaka huu.
Baadhi ya mashuhuda wamemwambia mwandishi wa habari hii kuwa baada ya wauaji kufanya unyama huo, waliuchukuwa mwili wake na kuuweka barabara kuu inayotoka Masasi- Lindi kwenda Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nyengedi, Thomas Ngomo, alikiri mlinzi huyo kuuawa na kwamba mwili wake uligunduliwa saa nane usiku na mtu aliyemtaja kuwa ni Abbas Kipengele, aliyekuwa akirejea kutoka Dar es Salaam kwenda Mtama.
“Taarifa ya kutokea mauaji ya mtu ni ya kweli. mwili wake ulikutwa na dereva wa lori aitwaye Kipengele akiwa anarejea kwao Mtama akitokea Dar es Salaam,” alisema Ngomo.
Alisema baada ya dereva Kipengele kuona hali hiyo, alitoa taarifa Kituo cha Polisi Mtama, ambao nao waliwaarifu wenzao kutoka wilayani na kufika kasha kuufanyia uchunguzi na kuukabidhi kwa ndugu na jamaa zake kwa ajili ya kwenda kuuzika.
Mtendaji huyo akasema licha ya kumchinja, watu hao walikatakata miguuni, maeneo ya kwenye magoti, kisha kutokomea kusikojulikana.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Mohamed Likwata, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kueleza kuwa hadi jana hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na kwamba askari wanaendelea na upelelezi ili kubaini waliohusika na hatimaye sheria kuchukuwa mkondo wake.

DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI

Post A Comment: