ads

BEKI wa Yanga, Hassan Kessy, amesema ataendelea kupambana na kuonyesha uwezo wake mazoezini ili kumshawishi kocha Mzambia George Lwandamina kumpa nafasi kikosi cha kwanza cha timu hiyo.


Kessy amejikuta akipoteza namba kikosi cha kwanza kufuatia kurejea kwa Juma Abdul ambaye kwa sasa anatumiwa na kocha huyo kwenye mechi za ligi.

Akizungumza  juzi, Kessy alisema kugombea namba kwenye timu ni jambo la kawaida na ni jukumu lake kumshawishi kocha wake ampange.

"Hakuna timu ambayo inakosa ushindani wa namba na jambo hilo ni zuri kwa sababu linaongeza hali ya kujituma, naamini nitapata nafasi ya kucheza tu," alisema Kessy.

Alisema anachokifanya sasa ni kujituma zaidi mazoezini na kufanya kile ambacho kocha wake anamwelekeza.

Kessy alikuwa kikosi cha kwanza wakati Abdul alipokuwa nje ya uwanja akiuguza majeraha na tangu aliporejea na kuonekana kuwa fiti amekuwa chaguo la kwanza kwenye mechi za mzunguko wa pili zilizopita.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: