MBUNGE wa zamani wa Kikwajuni, Parmuk Sing
Hogani, amesema haikuwa mwafaka Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC),
Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole,
Kuendelea kutetea msimamo wake wa muungano wa serikali tatu kwani kwa
sasa ni sehemu ya kiongozi wa chama hicho chenye msimamo wa muundo wa
serikali mbili.
Akizungumza mjini hapa jana, Hogani alisema sera ya CCM ni
muundo wa Muungano wa serikali mbili kuelekea moja, hivyo si mwafaka
kwa Polepole kuendele na msimamo wake wa serikali tatu kwa kile
alichoeleza unakwenda kinyume cha sera za chama chake.
“Kwa kuwa sasa ni kiongozi wa chama hatakiwi kuendelea kutetea
hadharani msimamo wake wakati akifahamu unakwenda kinyume cha sera ya
chama," alisema.
Hogani alisema CCM kwa kauli moja inapinga muundo wa Muungano wa
serikali tatu kama ilivyokuwa imependekezwa na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba kwa maslahi ya taifa, kulinda uhai wa Muungano wenyewe na
mashikamano wa wananchi.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: