RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein,
amevitaka vyuo vikuu vya Zanzibar kuisaidia Tume ya Kiswahili ya Afrika
Mashariki kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya mawasiliano katika nchi
wanachama wa jumuiya hiyo na kimataifa.
Dk. Shein alitoa wito huo alipokua akizungumza kwenye mahafali ya 16
ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Abdurahman Al-Sumait kilichopo Chukwani,
mkoa wa Mjini Magharibi Unguja mwishoni mwa wiki.
Alivitaka vyuo vikuu hivyo kufanya tafiti katika nyanja mbalimbali za
kiswahili na kutoa walimu wenye sifa ili kuendeleza lugha hiyo miongoni
mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na duniani.
“Ni muhimu kwa vyuo vikuu vyetu kuhakikisha mitaala yao inazingatia
mahitaji ya Tume ya Kiswahili ya Afrika Mashariki kwa sasa na baadaye,”
alisema Dk. Shein katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii, Mahmoud Thabit Kombo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: