HALI ya afya ya Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia aliyefanyiwa operesheni ya mguu
nchini India inaendelea vizuri na yupo nyumbani kwake Dar es Salaam
akiendelea na matibabu.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Juju Danda, Mbatia kwa sasa yupo nyumbani kwake Mbezi Beach akiendelea kujiuguza.
“Unajua kwa kuwa amefanyiwa operesheni, itachukua muda kurejea katika
hali yake ya kawaida, ila anaendelea vizuri kwa kweli na afya yake
inazidi kuimarika,” alisisitiza Danda.
Mbatia alifanyiwa operesheni ya mguu Novemba 14, mwaka huu katika
hospitali ya Zydus, India ambako alilazwa kuanzia Novemba 11 mwaka huu
baada ya kusumbuliwa na maradhi ya mguu.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: