MASHAHIDI wawili waliwasilisha ushahidi wao
wakati kesi ya tuhuma za unyang’anyi wa kutumia silaha, inayomkabili
Salum Njwete (34), maarufu ‘Scorpion’, iliponguruma kwenye Mahakama ya
Ilala jijini Dar es Salaam jana.
Kesi hiyo ambayo ‘Scorpion’ anadaiwa kumtoboa macho Said Ally, mkazi
wa Tabata jijini, ilianza majira ya saa 3:45 asubuhi hadi saa 5:10
mchana kwa shahidi wa pili na wa tatu kuwasilisha ushahidi wao. Shahidi
wa kwanza ni Ally ambaye aliwasilisha ushahidi wake Desemba 14, mwaka
huu.
Mashahidi wawili waliowasilisha ushahidi jana ni Stara Sudi, mke wa Ally na Yahaya Kisukari (23), mdogo wake na Ally.
Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Flora Haule, Wakili wa
Serikali, Nassoro Katuga na Wakili wa mshtakiwa, Juma Nassoro,
waliwauliza maswali mashahidi hao kwa nyakati tofauti huku kitendo cha
shahidi wa tatu (Kisukari) kudai kutopafahamu Buguruni kukionekana
kumshtua Wakili Nassoro ambaye alimuuliza shahidi mara tatu kuhusu
kulifahamu au kutolifahamu eneo hilo.
Shahidi huyo alidai hapajui Buguruni na hajawahi kufika katika eneo
hilo na endapo akipelekwa na mtu yoyote, atalazimika kushikwa mkono ili
asipotee ingawa kwa miaka minne anaishi eneo la Tabata lililopo jirani
na Buguruni.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: