KANISA Katoliki Jimbo la Morogoro ,limeipongeza Serikali ya Rais Dk
John Magufuli, kwa hatua inazoendelea kuchukua za uwajibikaji watumishi
wa umma , kujenga nidhamu na kuboresha huduma mbalimbali za kiuchumi na
kijamii.
Akizungumza jana baada ya kumaliza kuendesha misa takatifu ya sikukuu
ya Krisimasi nje ya Kanisa kuu la Mtakatifu Patrice la Jimbo la
Morogoro, Askofu Telesphor Mkude alisema kipindi cha mwaka mmoja tangu
Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani imeanza vizuri kwa kusimamia
nidhamu na uwajibikaji kwa watumishi wa umma.
Pia alisema, imesimamia vyema uboreshaji wa huduma za kijamii
zikiwemo za afya, miundombinu ya barabara na elimu ambazo ndani ya
kipindi hicho zinakwenda vizuri.
Aliongeza kuwa , Rais Magufuli ameonesha ujasiri kubwa katika
kusimamia uwajibikaji na nidhamu kwa watumishi wa umma ndani ya
Serikali. Hatua hiyo ni pamoja na kuona matumizi ya fedha za umma
zinazotokana na kodi za wananchi zinatumika katika kuhudumia huduma bora
za kijamii kwa Watanzania.
" Kila awamu inaanza namna yake, kwa mwaka mmoja wa serikali ya awamu
ya tano nadhani tunakwenda vizuri , huduma zinaonekana na zinapatikana
vizuri."
Hivyo alisema miongoni mwa ujasiri uliochukuliwa na Rais Dk Magufuli
katika serikali yake ni kulishughulikia suala la wafanyakazi wengi hewa
walikuwepo tangu awamu zilizomtangulia ambapo mabilioni ya fedha
yameokolewa na fedha hizo kuelekezwa katika huduma za jamii.
Askofu Mkude pia aliipongeza Serikali kwa kushughulikia na kuokoa
mabilioni mengine ya fedha zilikuwa zikitolewa na kulipwa wanafunzi hewa
kuanzia wa shule ya msingi hadi Vyuo Vikuu ambapo fedha hizo sasa
zimeelekezwa kuboresha huduma za jamii.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: