SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limetangaza kuwa watalipatia
Bunge la Tanzania laini ya umeme wa uhakika kutokana na mradi wa
backbone.
Hayo yalibainishwa na Msimamizi wa kituo cha kupozea umeme cha Zuzu
mjini Dodoma, Joseph Mongi alipokuwa akizungumza na wahariri
waliotembelea miradi ya umeme. Mongi alisema Bunge litapatiwa laini yao
ili kuliwezesha kuwa na umeme wa uhakika na wa kuaminika, tofauti na
ilivyo sasa kabla ya kuja kwa backbone.
“Dodoma tunazo laini maalumu kwa maeneo ya mashine za maji, ofisi za
serikali, chuo cha Udom, hospitali kuu ya mkoa na za wilaya za mkoa
huu,” alisema.
Alisema wamekidhi mahitaji na wanao uwezo wa kuhimili mahitaji ya
serikali yote ikihamia Dodoma. “Siyo mahitaji ya serikali mpya tu, bali
hata wawekezaji wa viwanda watakaohitaji kufungua viwanda katika makao
makuu ya Tanzania,” alisema.
Katika hatua nyingine, mradi mkubwa wa kusafirisha umeme wa backbone,
unaingia katika rekodi leo wakati laini nzima ya umeme huo
itakapowashwa. Meneja wa Ujenzi wa laini hiyo ya backbone, Oscar
Kanyama, alisema laini ya Dodoma hadi Singida inawashwa leo. Kanyama
alisema kwamba kuwashwa kwa kipande hicho, kutafanya mradi wote wa
kilovolti 400 kufanya kazi.
“Kesho tunawasha laini ya Dodoma hadi Singida na hivyo sasa laini
zote zitakuwa zinafanya kazi”, Kanyama aliwaeleza wahariri wanaotembelea
mradi huo kuanzia Iringa hadi Shinyanga. Mradi huo wenye urefu wa
kilometa 670, una vituo vinne vya kupozea umeme vya Iringa, Dodoma,
Singida na Shinyanga.
Laini za Iringa hadi Dodoma na Singida hadi Shinyanga, zilikuwa zimewashwa ikibaki ya Dodoma hadi Singida inayowashwa Leo.
Kanyama alisema kuwashwa kwa kipande hicho kutasaidia kuimarisha
upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya
Kaskazini.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: