![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemuona Askofu wa
Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima anayekabiliwa na kesi ya
kushindwa kuhifadhi silaha, ana kesi ya kujibu.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha alitoa uamuzi
huo jana baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi wa upande wa Jamhuri
pamoja na vielelezo.
Alisema kutokana na ushahidi huo, ameona upande wa Jamhuri umejenga
kesi hivyo Gwajima na wenzake watatu, wana haki ya kujitetea, kuita
mashahidi au kukaa kimya.
Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alidai kuwa washtakiwa watajitetea kwa njia ya kiapo na watakuwa na mashahidi watatu.
Hakimu Mkeha alisema Desemba 13, mwaka huu, washtakiwa watajitetea na
siku hiyo atasikiliza utetezi wa washtakiwa wote wanne pamoja na
mashahidi wao.
Mbali na Gwajima, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni msaidizi wa
askofu huyo, Yekonia Bihagaze (39), mfanyabiashara George Mnzava (43)
na mkazi wa Kimara Baruti, Geoffrey Milulu (31).
Inadaiwa kuwa, Machi 29 mwaka jana, katika Hospitali ya TMJ iliyopo
Mikocheni A, washitakiwa walikutwa wakimiliki bastola aina ya Baretta
yenye namba CAT 8802 bila kuwa na kibali kutoka mamlaka inayohusika na
silaha na milipuko.
Aidha, inadaiwa washtakiwa hao walikuwa wakimiliki isivyo halali
risasi tatu za bastola pamoja na risasi 17 za bunduki aina ya shotgun.
Gwajima anadaiwa kushindwa kuhifadhi silaha katika hali ya usalama.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: