RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amezipongeza Serikali ya
Oman na Cuba kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuendeleza
miradi ya maendeleo sambamba na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa
kihistoria uliopo kati ya nchi hizo.
Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati alipokutana na mabalozi wa
nchi hizo Ikulu mjini Unguja jana, Dk. Shein alizipongeza nchi hizo kwa
kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria ambao umekuwa chachu
katika kuimarisha juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika
kujileta maendeleo.
Akizungumza na Balozi wa Cuba anayemaliza muda wake wa kazi hapa
nchini, Jorge Tormo, walisisitiza haja ya kuendelea kuimarisha uhusiano
na ushirikiano kati ya pande mbili hizo.
Balozi Tormo alimuhakikikishia Dk. Shein kuwa Cuba inathamini sana
uhusiano na ushirikiano wa kihistoria kati yake na Zanzibar na kuahidi
kuendelea kuudumisha.
Alisema miradi yote ya maendeleo inayoishirikisha nchi yake
itaendelezwa kwa juhudi kubwa, huku akimweleza Dk. Shein kuwa nchi yake
itafarajika kwa kuwapo ushirikiano katika sekta ya utalii.
Mapema, Dk. Shein alifanya mazungumzo na Balozi mdogo mpya wa Oman,
Ahmed bin Humoud Al Habsi, na kutumia fursa hiyo kuipongeza nchi hiyo
kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika harakati zake za kukuza
uchumi na kuimarisha maendeleo.
Kwa upande wake, Balozi Al Habsi aliyechukua nafasi ya Balozi Ali
Abdulla Al Rashdi aliyemaliza muda wake wa kazi, alieleza kuwa Oman
itaendeleza uhusiano na ushirikiano wake na Zanzibar na kupongeza hatua
za maendeleo zilizofikiwa hapa nchini.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: