Waziri wa muda mrefu
na mbunge wa zamani wa Bunda, Steven Wasira amewajibu wanaodai kwamba
amelazimika kustaafu siasa baada ya mpinzani wake, Ester Bulaya
kuwashinda wapigakura wanne waliokuwa wakipinga ushindi wake wa ubunge
wa Bunda Mjini na kusema hajastaafu na uzee haumzuii mtu kudai haki
yake.
Juzi,
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilimpa ushindi Bulaya katika kesi ya
uchaguzi hali iliyotafsiriwa na wadadisi wa kisiasa kwamba huo ndiyo
ulikuwa mwisho wa kisiasa wa Wasira.
Lakini
jana, Wasira alipopigiwa simu na waandishi wetu kuelezea hatima yake ya
kisiasa baada ya kesi hiyo, alisema wanaodai kuwa anatakiwa kustaafu
siasa kwa sababu ni mzee hawana budi kuangalia kauli zao kwa sababu wapo
wazee wengi anaowafahamu kwa majina na bado wapo madarakani.
“Suala
la kusema nimestaafu siasa silijui na sijawahi kusema. Kesi hiyo
inahusiana nini na siasa? Wapigakura wameona kuwa uchaguzi haukuwa huru
na haki. Hakuna uhusiano na uhusiano uliopo ni kwa sababu mimi ni
shahidi na mimi niligombea,” alisema na kuongeza:
“Nataka
wanipe ‘definition’ (maana) ya kustaafu siasa. Je, ni kunyamaza,
nisitoe maoni. Mbona wapo watu walikuwa wanasiasa na bado wanatoa maoni
ya kisiasa tena yenye manufaa makubwa?”
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: