Nyota
Cristiano Ronaldo amerudi kwa kasi akifumania nyavu kwa kishindo, baada
ya kufunga mabao matatu (hat trick) na kuiwezesha Real Madrid kuilaza
Atletico Madrid kwa 3-0 katika uwanja wa Vicente Calderon kuamkia leo.
Kwa
mantiki hiyo, Madrid imejiimarisha kileleni kwa tofauti ya pointi nne
dhidi ya mahasimu wao Barcelona, ambayo awali ililazimishwa sare ya bila
kufungana na Malaga.
Zikiwa
zimecheza michezo sawa, Real Madrid inaongoza baada ya kujikusanyia
pointi 30, ikifuatiwa na Barcelona yenye alama 26 huku Atletico Madrid
ikisalia na pointi 24.
Ronaldo
alianza kutikisa nyavu katika dakika ya 23 baada ya kupiga mkwaju wa
adhabu na kuwababatiza mabeki wa Atletico. Alizidi kuwapa furaha
mashabiki wa Madrid baada ya kufunga kwa njia ya penalti dakika ya 71
kabla ya kukamilisha hat-trick katika dakika ya 77, baada ya kuunganisha
krosi safi iliyopigwa na winga mwenye mbio, Gareth Bale.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI



Post A Comment: